9 Hakuna tena kunywa divai na kuimba;mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji.
10 Mji uliohamwa umejaa uharibifu;kila nyumba imefungwa asiingie mtu.
11 Kuna kilio barabarani kwa kukosa divai;shangwe yote imekoma,furaha imetoweka duniani.
12 Mji ni magofu matupu;malango yake yamevunjwavunjwa.
13 Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituniau tini chache tu juu ya mtinibaada ya kumaliza mavuno,ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote:Watu wachache watabakia hai.
14 Watakaosalia watapaza sauti,wataimba kwa shangwe.Kutoka magharibi watatangaza ukuu wa Mwenyezi-Mungu,
15 nao wakazi wa mashariki watamsifu.Watu wa mbali watalisifujina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.