12 Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake,kuzipima mbingu kwa mikono yake?Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni;kuipima milima kwa mizaniau vilima kwa kipimo cha uzani?
13 Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu,au kuwa mshauri wake na kumfunza?
14 Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri,ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi?Nani aliyemfunza njia za haki?Nani aliyemfundisha maarifa,na kumwonesha namna ya kuwa na akili?
15 Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo,ni kama vumbi juu ya mizani.Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
16 Kuni zote za Lebanonina wanyama wake wotehavitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.
17 Mataifa yote si kitu mbele yake;kwake ni vitu duni kabisa na batili.
18 Mtamlinganisha Mungu na nini basi,au ni kitu gani cha kumfananisha naye?