1 Mtu mwadilifu akifa,hakuna mtu anayejali;mtu mwema akifariki,hakuna mtu anayefikiri na kusema:“Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa,
2 ili apate kuingia kwenye amani.”Watu wanaofuata njia ya haki,watakuwa na amani na kupumzika.
3 Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Njoni hapa nyinyi wana wa wachawi;nyinyi wazawa wa wachawi, wazinzi na malaya.
4 Je, mnadhani mnamdhihaki nani?Mnamfyonya nani na kumtolea ulimi?Nyinyi wenyewe ni wahalifu tangu mwanzo,nyinyi ni kizazi kidanganyifu.
5 Nyinyi mnawaka tamaa kwenye miti ya mialoni,na katika kila mti wa majani mabichi.Mnawachinja watoto wenuna kuwatambika katika mabonde na nyufa za majabali.
6 Mnachagua mawe laini mabondeni,na kuyafanya kitovu cha maisha yenu.Mnayamiminia tambiko ya kinywajina kuyapelekea tambiko ya nafaka!Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?