16 Aliona kwamba hakuna mtu aliyejali,akashangaa kwamba hakuna aliyeingilia kati.Basi akaamua kunyosha mkono wake mwenyewe,uadilifu wake ukamhimiza.
17 Alivaa uadilifu kama vazi la kujikinga kifuani,na wokovu kama kofia ya chuma kichwani.Atajivika kisasi kama vazi,na kujifunika wivu kama joho.
18 Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao,naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake;atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.
19 Toka magharibi hadi mashariki,kila mtu atamcha Mwenyezi-Munguna kutambua utukufu wake.Maana atakuja kama mto uendao kasi,mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.
20 Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi,Mkombozi wa wazawa wa Yakoboambao wataachana na makosa yao.Asema Mwenyezi-Mungu.
21 Mwenyezi-Mungu asema:“Mimi nafanya nanyi agano hili:Roho yangu niliyowajazeni,maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu,hayataondoka kwenu kamwe,wala kwa watoto na wajukuu zenu,tangu sasa na hata milele.”