4 Sauti yao iliitikisa misingi ya milango ya hekalu, nalo likajaa moshi.
5 Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
6 Basi, mmoja wa hao malaika akaruka kunijia, akiwa ameshika mkononi koleo lililokuwa na kaa la moto alilolitwaa madhabahuni.
7 Naye akinigusa nalo mdomoni, akasema: “Tazama, kaa hili limekugusa mdomo; umeondolewa hatia yako, umesamehewa dhambi yako.”
8 Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi.”
9 Naye akaniambia, “Nenda ukawaambie watu hawa:‘Mtasikiliza sana, lakini hamtaelewa;mtatazama sana, lakini hamtaona.’”
10 Kisha akaniambia,“Zipumbaze akili za watu hawa,masikio yao yasisikie,macho yao yasione;ili wasije wakaona kwa macho yao,wakasikia kwa masikio yao,wakaelewa kwa akili zao,na kunigeukia, nao wakaponywa.”