12 Mnapokuja mbele yangu kuniabudunani aliyewataka mkanyagekanyage nyua zangu?
13 Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana;ubani ni chukizo kwangu.Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya,Sabato na mikutano mikubwa ya ibada;sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezomoyo wangu wazichukia.Zimekuwa mzigo mzito kwangu,nami nimechoka kuzivumilia.
15 “Mnapoinua mikono yenu kuombanitauficha uso wangu nisiwaone.Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,maana mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, jitakaseni;ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu.Acheni kutenda maovu,
17 jifunzeni kutenda mema.Tendeni haki,ondoeni udhalimu,walindeni yatima,teteeni haki za wajane.”
18 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Njoni, basi, tuhojiane.Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,mtakuwa weupe kama sufu.