4 Sikilizeni kelele milimanikama za kundi kubwa la watu!Sikilizeni kelele za falme,na mataifa yanayokusanyika!Mwenyezi-Mungu wa majeshianalikagua jeshi linalokwenda vitani.
5 Wanakuja kutoka nchi za mbali,wanatoka hata miisho ya dunia:Mwenyezi-Mungu na silaha za hasira yakeanakuja kuiangamiza dunia.
6 Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia;inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu.
7 Kwa hiyo mikono ya kila mtu italegea,kila mtu atakufa moyo.
8 Watu watafadhaika,watashikwa na hofu na maumivu,watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua.Watatazamana kwa mashaka,nyuso zao zitawaiva kwa haya.
9 Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,siku kali, ya ghadhabu na hasira kali.Itaifanya nchi kuwa uharibifu,itawaangamiza wenye dhambi wake.
10 Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza;jua linapochomoza litakuwa giza,na mwezi hautatoa mwanga wake.