4 Je, mnadhani mnamdhihaki nani?Mnamfyonya nani na kumtolea ulimi?Nyinyi wenyewe ni wahalifu tangu mwanzo,nyinyi ni kizazi kidanganyifu.
5 Nyinyi mnawaka tamaa kwenye miti ya mialoni,na katika kila mti wa majani mabichi.Mnawachinja watoto wenuna kuwatambika katika mabonde na nyufa za majabali.
6 Mnachagua mawe laini mabondeni,na kuyafanya kitovu cha maisha yenu.Mnayamiminia tambiko ya kinywajina kuyapelekea tambiko ya nafaka!Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
7 Mmeweka vitanda vyenu juu ya milima mikubwa,na kwenda huko kutoa tambiko.
8 Nyuma ya milango na miimommetundika kinyago chenu.Nyinyi mnaniacha mimina kutandika na kuvipanua vitanda vyenu.Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao.Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya,huku mnakodolea macho kinyago chenu.
9 Mnajitia marashi na manukato kwa wingikisha mnakwenda kumwabudu Moleki.Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko,kujitafutia miungu ya kuabudu;hata kuzimu walifika.
10 Mlichoshwa na safari zenu ndefu,hata hivyo hamkukata tamaa;mlijipatia nguvu mpya,ndiyo maana hamkuzimia.