1 Kwa ajili ya Siyoni sitakaa kimya,kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,mpaka kuokolewa kwake kuchomoze kama umeme,wokovu wake utokeze kama mwenge.
2 Mataifa watauona wokovu wako,wafalme wote watauona utukufu wako.Nawe utaitwa kwa jina jipya,jina atakalokupa Mwenyezi-Mungu mwenyewe.
3 Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu;kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
4 Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”,wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”.Bali utaitwa: “Namfurahia,”na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.”Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe,naye atakuwa kama mume wa nchi yako.
5 Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana,ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako.Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi,ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako.