14 Watumishi wangu wataimba kwa furaha moyoni,lakini nyinyi mtalia kwa uchungu moyonina kupiga kelele kwa uchungu mkubwa rohoni.
15 Wale niliowachagua nitawapa jina jipya.Lakini nyinyi jina lenu watalitumia kulaania;‘Watasema: Bwana Mungu awaue kama hao.’
16 Basi, mwenye kujitakia baraka nchini,atajitakia baraka kwa Mungu wa kweli.Mwenye kuapa katika nchi hii,ataapa kwa Mungu wa kweli.Maana taabu za zamani zimepitazimetoweka kabisa mbele yangu.
17 “Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya.mambo ya zamani hayatakumbukwa tena.
18 Furahini, mkashangilie milele,kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba.Yerusalemu nitaufanya mji wa shangwe,na watu wake watu wenye furaha.
19 Nami nitaufurahia mji wa Yerusalemu,nitawafurahia watu wangu.Sauti ya kilio haitasikika tena,kilio cha taabu hakitakuwako.
20 Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga,wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao.Akifa mtu wa miaka 100 amekufa akiwa kijana;na akifa kabla ya miaka 100 ni balaa.