21 Watu watajenga nyumba na kuishi humo;watalima mizabibu na kula matunda yake.
22 Hawatajenga nyumba zikaliwe na watu wengine,wala kulima chakula kiliwe na watu wengine.Maana watu wangu niliowachaguawataishi maisha marefu kama miti;wateule wangu watafurahia matunda ya jasho lao.
23 Kazi zao hazitakuwa bure,wala hawatazaa watoto wa kupata maafa;maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu,wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.
24 Hata kabla hawajaniita, mimi nitawaitikia;kabla hawajamaliza kusema, nitakuwa nimewajibu.
25 Mbwamwitu na kondoo watakula pamoja,simba watakula nyasi kama ng'ombe,nao nyoka chakula chao kitakuwa vumbi.Katika mlima wangu wote mtakatifu,hakuna atakayeumiza au kuharibu kitu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”