7 Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”
8 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri,watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;sitawaangamiza wote.
9 Nitawajalia watu wa Yakobo,na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu;watumishi wangu watakaa huko.
10 Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho,bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugokwa ajili ya watu wangu walionitafuta.
11 “Lakini nitafanya nini na nyinyimnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu,msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu,nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’,na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’?
12 Nimewapangia kifo kwa upanga,nyote mtaangukia machinjoni!Maana, nilipowaita, hamkuniitikia;niliponena, hamkunisikiliza.Mlitenda yaliyo maovu mbele yangu,mkachagua yale nisiyoyapenda.
13 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema,watumishi wangu watakula,lakini nyinyi mtaona njaa;watumishi wangu watakunywa,lakini nyinyi mtaona kiu;watumishi wangu watafurahi,lakini nyinyi mtafedheheka.