3 Ngombe humfahamu mwenyewe,punda hujua kibanda cha bwana wake;lakini Waisraeli hawajui,watu wangu, hawaelewi!”
4 Ole wako wewe taifa lenye dhambi,watu waliolemewa na uovu,wazawa wa wenye kutenda maovu,watu waishio kwa udanganyifu!Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu,mmemdharau Mtakatifu wa Israeli,mmefarakana naye na kurudi nyuma.
5 Kwa nini huachi uasi wako?Mbona wataka kuadhibiwa bado?Kichwa chote ni majeraha matupu,na moyo wote unaugua!
6 Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu,umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu,navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
7 Nchi yenu imeharibiwa kabisa;miji yenu imeteketezwa kwa moto.Wageni wananyakua nchi yenu mkiona kwa macho,imeharibiwa kama uharibifu wa Sodoma.
8 Mji Siyoni umeachwa kama kibanda shambani,kama kitalu katika shamba la matango,kama mji uliozingirwa.
9 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asingalituachia wachache,tungalikwisha kuwa kama watu wa Sodoma,tungalikuwa hali ileile ya Gomora.