6 Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu,umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu,navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
7 Nchi yenu imeharibiwa kabisa;miji yenu imeteketezwa kwa moto.Wageni wananyakua nchi yenu mkiona kwa macho,imeharibiwa kama uharibifu wa Sodoma.
8 Mji Siyoni umeachwa kama kibanda shambani,kama kitalu katika shamba la matango,kama mji uliozingirwa.
9 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asingalituachia wachache,tungalikwisha kuwa kama watu wa Sodoma,tungalikuwa hali ileile ya Gomora.
10 Sikilizeni neno la Mwenyezi-Munguenyi watawala waovu kama wa Sodoma!Sikilizeni mafunzo ya Mungu wetuenyi watu waovu kama wa Gomora!
11 Mwenyezi-Mungu asema hivi;“Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu?Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwana mafuta ya wanyama wenu wanono.Sipendezwi na damu ya fahali,wala ya wanakondoo, wala ya beberu.
12 Mnapokuja mbele yangu kuniabudunani aliyewataka mkanyagekanyage nyua zangu?