4 Wakimbizi wa Moabu waishi kwenu,muwe kimbilio lao mbali na mwangamizi.”Mdhalimu atakapokuwa ametoweka,udhalimu utakapokuwa umekoma,na wavamizi kutoweka nchini,
5 utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi,mtawala apendaye kutenda haki,na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa;atatawala humo kwa uaminifu.
6 Watu wa Yuda wanasema hivi:“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu,tunajua jinsi alivyojivuna mno;tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake;lakini majivuno yake hayo ni bure.”
7 Sasa Wamoabu wanalia;wote wanaomboleza juu ya nchi yao.Ombolezeni kwa pigo hilo kubwa,na juu ya maandazi ya zabibu za Kir-haresethi.
8 Mashamba ya Heshboni yamefifia.Kadhalika na zabibu za Sibmaambazo ziliwalevya wakuu wa mataifazikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani,chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.
9 Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazerikwa ajili ya mizabibu ya Sibma.Machozi yananitoka kwa ajili yenu,enyi miji ya Heshboni na Eleale;maana vigelegele vya mavuno ya matunda,vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.
10 Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba.Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena,wala kupiga vigelegele.Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni,sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.