1 Ole, wake nchi iliyojaa mvumo wa mabawa,nchi iliyoko ngambo ya mito ya Kushi!
2 Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili,wamepanda mashua za mafunjo.Nendeni, enyi wajumbe wepesi,kwa taifa kubwa na hodari,la watu warefu na wa ngozi laini.Watu hao wanaoogopwa kila mahalina nchi yao imegawanywa na mito.
3 Enyi wakazi wote ulimwenguni,nanyi mkaao duniani!Ishara itakapotolewa mlimani, tazameni!Tarumbeta itakapopigwa, sikilizeni.
4 Maana, Mwenyezi-Mungu ameniambia hivi:“Toka makao yangu juu nitatazama yanayotukia,nimetulia kama joto katika mwanga wa jua,kama wingu la umande wakati wa mavuno.
5 Maana, kabla ya mavuno,wakati wa kuchanua umekwisha,maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu,Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea,na kuyakwanyua matawi yanayotanda.
6 Yote yataachiwa ndege milimani,na wanyama wengine wa porini.Ndege walao nyama watakaa humowakati wa majira ya kiangazi,na wanyama wa porini watafanya makao humowakati wa majira ya baridi.”