4 Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha,niwatie moyo wale waliochoka.Kila asubuhi hunipa hamuya kusikiliza anayotaka kunifunza.
5 Bwana Mungu amenifanya msikivu,nami sikuwa mkaidiwala kugeuka mbali naye.
6 Mgongo wangu niliwaachia walionipiga,mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu;walioniaibisha na kunitemea mate,sikujificha mbali nao.
7 Bwana Mungu hunisaidia,kwa hiyo siwezi kufadhaika.Uso wangu nimeukaza kama jiwe;najua kwamba sitaaibishwa.
8 Mtetezi wangu yuko karibu.Ni nani atakayepingana nami?Na aje tusimame mahakamani.Adui yangu ni nani?Na ajitokeze mbele basi.
9 Tazama Bwana Mungu hunisaidia.Ni nani awezaye kusema nina hatia?Maadui zangu wote watachakaa kama vazi,nondo watawatafuna.
10 Nani kati yenu amchaye Mwenyezi-Mungu?Nani anayetii maneno ya mtumishi wake?Kama yupo atembeaye gizani bila taa,amtumainie Mwenyezi-Mungu,na kumtegemea Mungu wake.