15 Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa,aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”:“Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu,nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu.Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevuna kuwapa nguvu wenye majuto.
16 Maana sitaendelea kuwalaumuwala kuwakasirikia daima.La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu,nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai.
17 Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao;niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika.Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
18 Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya;nitawaongoza na kuwapa faraja,nitawatuliza hao wanaoomboleza.
19 Mimi nitawapa amani,amani kwa walio mbali na walio karibu!Mimi nitawaponya.
20 Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka,ambayo haiwezi kutulia;mawimbi yake hutupa tope na takataka.”
21 Mungu wangu asema hivi:“Watu waovu sitawapa amani.”