1 Mwenyezi-Mungu asema:“Piga kelele, wala usijizuie;paza sauti yako kama tarumbeta.Watangazie watu wangu makosa yao,waambie wazawa wa Yakobo dhambi zao.
2 Siku hata siku wananijia kuniabudu,wanatamani kujua mwongozo wangu,kana kwamba wao ni taifa litendalo haki,taifa lisilosahau sheria za Mungu wao.Wananitaka niamue kwa haki,na kutamani kukaa karibu na Mungu.
3 “Nyinyi mnaniuliza:‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni?Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’“Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga,mnatafuta tu furaha yenu wenyewe,na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!
4 Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi.Mkifunga namna hiyomaombi yenu hayatafika kwangu juu.
5 Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha;mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi,na kulalia nguo za magunia na majivu.Je, huo ndio mnaouita mfungo?Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
6 “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:Kuwafungulia waliofungwa bila haki,kuziondoa kamba za utumwa,kuwaachia huru wanaokandamizwa,na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
7 Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.