1 Heri mtu asiyefuata shauri la waovu,asiyeshiriki njia za wenye dhambi,wala kujumuika na wenye dharau;
2 bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu,na kuitafakari mchana na usiku.
3 Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito,unaozaa matunda kwa wakati wake,na majani yake hayanyauki.Kila afanyalo hufanikiwa.
4 Lakini waovu sivyo walivyo;wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu,wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu.
6 Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu;lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi.