1 Kama paa atamanivyo maji ya kijito,ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!
2 Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai.Nitafika lini kwake na kuuona uso wake?
3 Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,waliponiambia kila siku: “Yuko wapi Mungu Wako!”
4 Nakumbuka tena mambo hayakwa majonzi moyoni mwangu:Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Munguwakipiga vigelegele vya shukrani;umati wa watu wakifanya sherehe!
5 Mbona nasononeka hivyo moyoni?Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu?Nitamtumainia Mungu,maana nitamsifu tenayeye aliye msaada wangu na Mungu wangu.
6 Nimesongwa na huzuni moyoni mwangu,kwa hiyo ninakukumbuka wewe, ee Mungu,kutoka katika eneo la Yordani,kutoka mlima Hermoni na Mizari.
7 Nimeporomoshewa mafuriko ya majimafuriko ya maji yaja karibunayo yaita maporomoko mapya.Mawimbi na mapigo yako yamenikumba.
8 Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana;nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku,nimwombe Mungu anipaye uhai.
9 Namwambia Mungu, mwamba wangu:“Kwa nini umenisahau?Yanini niende huko na huko nikiombolezakwa kudhulumiwa na adui yangu?”
10 Nimepondwa kwa matukano yao,wanaponiuliza kila siku:“Yuko wapi, Mungu wako!”
11 Mbona nasononeka hivyo moyoni?Kwa nini nahangaika hivyo?Nitamtumainia Mungu,maana nitamsifu tena Mungu,aliye msaada wangu na Mungu wangu.