1 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake,mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.
2 Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia,mtu ambaye hana hila moyoni mwake.
3 Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu,nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.
4 Mchana na usiku mkono wako ulinilemea;nikafyonzwa nguvu zangu,kama maji wakati wa kiangazi.
5 Kisha nilikiri makosa yangu kwako;wala sikuuficha uovu wangu.Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu,ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote.
6 Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi;jeshi likaribiapo au mafuriko,hayo hayatamfikia yeye.
7 Wewe ndiwe kinga yangu;wewe wanilinda katika taabu.Umenijalia shangwe za kukombolewa.
8 Mungu asema: “Nitakufunzana kukuonesha njia unayopaswa kufuata.Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
9 Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,la sivyo hawatakukaribia.”
10 Watu waovu watapata mateso mengi,bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.
11 Furahini na kushangilia kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu;pigeni vigelegele vya shangwe enyi wanyofu wa moyo.