1 Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu,sitapungukiwa na kitu.
2 Hunipumzisha kwenye malisho mabichi;huniongoza kando ya maji matulivu,
3 na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya.Huniongoza katika njia sawakwa hisani yake.
4 Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo,sitaogopa hatari yoyote,maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami;gongo lako na fimbo yako vyanilinda.
5 Umeniandalia karamu mbele ya maadui zangu;umenipaka mafuta kichwani pangu;kikombe changu umekijaza mpaka kufurika.
6 Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami,siku zote za maisha yangu;nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.