1 Wapumbavu hujisemea moyoni:“Hakuna Mungu.”Wote wamepotoka kabisa,wametenda mambo ya kuchukiza;hakuna hata mmoja atendaye jema!
2 Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni,aone kama kuna yeyote mwenye busara,kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.
3 Lakini wote wamekosa,wote wamepotoka pamoja;hakuna atendaye mema,hakuna hata mmoja.
4 “Je, hao watendao maovu hawana akili?Wanawatafuna watu wangu kama mikate;wala hawanijali mimi Mwenyezi-Mungu.”
5 Hapo watashikwa na hofu kubwa,maana Mungu yu pamoja na waadilifu.
6 Unaweza kuvuruga mipango ya maskini,lakini Mwenyezi-Mungu ndiye kimbilio lake.
7 Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni!Mwenyezi-Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake,wazawa wa Yakobo watashangilia;Waisraeli watafurahi.