1 Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako?Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu?
2 Ni mtu aishiye bila lawama,atendaye daima yaliyo mema,asemaye ukweli kutoka moyoni;
3 ni mtu asiyesengenya watu,asiyemtendea uovu rafiki yake,wala kumfitini jirani yake;
4 ni mtu anayewadharau wafisadi,lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu;ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara;
5 asiyekopesha fedha yake kwa riba,wala kupokea rushwa kumdhulumu asiye na hatia.Mtu atendaye hayo,kamwe hatatikisika.