1 Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu,ni wengi mno hao wanaonishambulia.
2 Wengi wanasema juu yangu,“Hatapata msaada kwa Mungu.”
3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande;kwako napata fahari na ushindi wangu.
4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu,nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.
5 Nalala na kupata usingizi,naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza.
6 Sitayaogopa maelfu ya watu,wanaonizingira kila upande.
7 Uje ee Mwenyezi-Mungu!Niokoe ee Mungu wangu!Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote;wawavunja meno waovu wasinidhuru.
8 Mwenyezi-Mungu ndiwe uokoaye;uwape baraka watu wako.