1 Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako,anafurahi mno kwa msaada uliompa.
2 Umemtimizia matakwa ya moyo wake;wala hukumkatalia ombi lake.
3 Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri;umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.
4 Alikuomba maisha nawe ukampa;ulimpa maisha marefu milele na milele.
5 Kwa msaada wako ametukuka sana;wewe umemjalia fahari na heshima.
6 Wamjalia baraka zako daima;wamfurahisha kwa kuwako kwako.
7 Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu;kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.
8 Mkono wako ewe mfalme utawakamata maadui zako wote;mkono wako wa kulia utawakamata wanaokuchukia.
9 Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto.Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake,moto utawateketeza kabisa.
10 Utawaangamiza wazawa wao kutoka duniani;watoto wao hawatasalia kati ya binadamu.
11 Hata kama wakipanga maovu dhidi yako,kama wakitunga mipango ya hila,kamwe hawataweza kufaulu.
12 Kwa maana wewe utawatimua mbio,utawalenga usoni kwa mishale yako.
13 Utukuzwe ee Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya nguvu yako!Tutaimba na kuusifu uwezo wako.