1 Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama;mnawezaje basi kuniambia:“Ruka kama ndege, mpaka milimani,
2 maana waovu wanavuta pinde;wameweka mishale tayari juu ya uta,wawapige mshale watu wema gizani!
3 Kama misingi ikiharibiwa,mtu mwadilifu atafanya nini?”
4 Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu;kiti cha enzi cha Mwenyezi-Mungu kiko mbinguni.Kwa macho yake huwachungulia wanadamu,na kujua kila kitu wanachofanya.
5 Mwenyezi-Mungu huwapima waadilifu na waovu;huwachukia kabisa watu wakatili.
6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti;upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.
7 Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu;watu wanyofu watakaa pamoja naye.