1 Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni;jina la Mungu wa Yakobo likulinde.
2 Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake;akutegemeze kutoka mlima Siyoni.
3 Azikumbuke sadaka zako zote;azikubali tambiko zako za kuteketezwa.
4 Akujalie unayotamani moyoni mwako,aifanikishe mipango yako yote.
5 Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako;tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu.Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!
6 Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua,atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni;kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.
7 Wengine hujigamba kwa magari ya vita;wengine hujigamba kwa farasi wao.Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
8 Hao watajikwaa na kuanguka;lakini sisi tutainuka na kusimama imara.
9 Umjalie mfalme ushindi, ee Mwenyezi-Mungu;utujibu wakati tunapokuomba.