1 Kwa nini mataifa yanafanya ghasia?Mbona watu wanafanya njama za bure?
2 Wafalme wa dunia wanajitayarisha;watawala wanashauriana pamoja,dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake.
3 Wanasema: “Tujiondoe katika utawala wao;tutupilie mbali minyororo yao!”
4 Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni,anawacheka na kuwadhihaki.
5 Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu,na kuwatisha kwa hasira, akisema:
6 “Nimemtawaza mfalme niliyemteua,anatawala Siyoni, mlima wangu mtakatifu!”
7 Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu.Mungu aliniambia:‘Wewe ni mwanangu,mimi leo nimekuwa baba yako.
8 Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako,na dunia nzima kuwa mali yako.
9 Utawaponda kwa fimbo ya chuma;utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’”
10 Sasa enyi wafalme, tumieni busara;sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia.
11 Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji;
12 msujudieni na kutetemeka;asije akakasirika, mkaangamia ghafla;kwani hasira yake huwaka haraka.Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!