1 Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu!Watu wema wamekwisha;waaminifu wametoweka miongoni mwa watu.
2 Kila mmoja humdanganya mwenzake,husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki.
3 Ee Mwenyezi-Munguuikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu,na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia.
4 Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo tunayo, nani awezaye kututawala?”
5 Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Kwa sababu maskini wanadhulumiwa,na wahitaji wanapiga kite, sasa naja,nami nitawapa usalama wanaoutazamia.”
6 Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi,safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri,naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
7 Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu,utukinge daima na kizazi hiki kiovu.
8 Waovu wanazunguka kila mahali;upotovu unatukuzwa kati ya watu.