1 Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu!Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi,la sivyo kama usiponisikiliza,nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.
2 Sikiliza sauti ya ombi langu,ninapokulilia unisaidie,ninapoinua mikono yangu kuelekea maskani yako takatifu.
3 Usinipatilize pamoja na watu wabaya,pamoja na watu watendao maovu:Watu wasemao na wenzao maneno ya amani,kumbe wamejaa uhasama moyoni.
4 Uwaadhibu kadiri ya matendo yao,kufuatana na maovu waliyotenda.Waadhibu kadiri ya matendo yao wenyewe;uwatendee yale wanayostahili.
5 Hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu;hawatambui mambo aliyoyafanya.Kwa sababu hiyo atawabomoa,wala hatawajenga tena upya.
6 Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,maana amesikiliza ombi langu.
7 Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu;tegemeo la moyo wangu limo kwake.Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo;kwa wimbo wangu ninamshukuru.
8 Mwenyezi-Mungu ni nguvu ya watu wake;yeye ni kimbilio la wokovu kwa mfalme wake mteule.
9 Ee Mungu, uwaokoe watu wako;uwabariki watu hao walio mali yako.Uwe mchungaji wao na kuwategemeza milele.