1 Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu,ni nani nitakayemwogopa?Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu,sitamwogopa mtu yeyote.
2 Waovu wakinishambulia,na kutaka kuniangamiza,hao wapinzani wangu watajikwaa na kuanguka.
3 Hata jeshi likinizunguka,moyo wangu hautaogopa kitu;hata nikikabiliwa na vita,bado nitakuwa na tumaini.
4 Jambo moja nimemwomba Mwenyezi-Mungu,nalo ndilo ninalolitafuta:Nikae nyumbani mwa Mwenyezi-Mungusiku zote za maisha yangu;niuone uzuri wake Mwenyezi-Mungu,na kutafuta maongozi yake hekaluni mwake.
5 Siku ya taabu atanificha bandani mwake;atanificha katika hema lake,na kunisalimisha juu ya mwamba.
6 Nami kwa fahari nitaangalia juuya maadui zangu wanaonizunguka.Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake,nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.
7 Usikie, ee Mwenyezi-Mungu, ninapokulilia,unionee huruma na kunijibu.
8 Moyo wangu waniambia: “Njoo umtafute Mungu!”Basi, naja kwako, ee Mwenyezi-Mungu.
9 Usiache kuniangalia kwa wema.Usinikatae kwa hasira mimi mtumishi wako;wewe umekuwa daima msaada wangu.Usinitupe wala usiniache, ee Mungu Mwokozi wangu.
10 Hata kama wazazi wangu wakinitupa,Mwenyezi-Mungu atanipokea kwake.
11 Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu;uniongoze katika njia iliyo sawa,kwa sababu ya maadui zangu.
12 Usiniache maadui wanitende wapendavyo;maana mashahidi wa uongo wananikabili,nao wanatoa vitisho vya ukatili.
13 Naamini nitauona wema wake Mwenyezi-Mungukatika makao ya walio hai.
14 Mtegemee Mwenyezi-Mungu!Uwe na moyo, usikate tamaa!Naam, mtegemee Mwenyezi-Mungu!