1 Dhambi huongea na mtu mwovu,ndani kabisa moyoni mwake;jambo la kumcha Mungu halimo kabisa kwake.
2 Mwovu hujipendelea mwenyewe,hufikiri uovu wake hautagunduliwa na kulaaniwa.
3 Kila asemacho ni uovu na uongo;ameacha kutumia hekima na kutenda mema.
4 Alalapo huwaza kutenda maovu,hujiweka katika njia isiyo njema,wala haachani na uovu.
5 Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni;uaminifu wako wafika mawinguni.
6 Uadilifu wako ni kama milima mikubwa,hukumu zako ni kama vilindi vya bahari.Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama
7 Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako!Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako.
8 Wawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako;wawanywesha kutoka mto wa wema wako.
9 Wewe ndiwe asili ya uhai;kwa mwanga wako twaona mwanga.
10 Uendelee kuwafadhili wale wanaokutambua;uzidi kuwa mwema kwa wanyofu wa moyo.
11 Usikubali wenye majivuno wanivamie,wala watu waovu wanikimbize.
12 Kumbe watendao maovu wameanguka;wameangushwa chini, hawawezi kuinuka.