1 Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu!Watu wema wamekwisha;waaminifu wametoweka miongoni mwa watu.
2 Kila mmoja humdanganya mwenzake,husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki.
3 Ee Mwenyezi-Munguuikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu,na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia.
4 Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo tunayo, nani awezaye kututawala?”