1 Shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu!Kumsifu Mungu ni wajibu wa watu wanyofu.
2 Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa zeze;mwimbieni kwa kinubi cha nyuzi kumi.
3 Mwimbieni wimbo mpya;pigeni kinubi vizuri na kushangilia.
4 Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli;na matendo yake yote ni ya kuaminika.
5 Mungu apenda uadilifu na haki,dunia imejaa fadhili za Mwenyezi-Mungu.