18 Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao,watu ambao wanatumainia fadhili zake.
19 Yeye huwaokoa katika kifo,huwaweka hai wakati wa njaa.
20 Mioyo yetu yamtumainia Mwenyezi-Mungu.Yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21 Naam twafurahi kwa sababu yake;tuna matumaini katika jina lake takatifu.
22 Fadhili zako zikae nasi, ee Mwenyezi-Mungu,kwani sisi tumekuwekea tumaini letu.