2 Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa zeze;mwimbieni kwa kinubi cha nyuzi kumi.
3 Mwimbieni wimbo mpya;pigeni kinubi vizuri na kushangilia.
4 Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli;na matendo yake yote ni ya kuaminika.
5 Mungu apenda uadilifu na haki,dunia imejaa fadhili za Mwenyezi-Mungu.
6 Mbingu ziliumbwa kwa neno la Mwenyezi-Mungu,na vyote vilivyomo kwa pumzi ya mdomo wake.
7 Alikusanya maji ya bahari kama katika chupa,vilindi vya bahari akavifunga ghalani.
8 Dunia yote na imwogope Mwenyezi-Mungu!Wakazi wote duniani, wamche!