1 Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo.Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia;unionee huruma na kusikia sala yangu.
2 Jamani, mtaniharibia jina langu mpaka lini?Mpaka lini mtapenda upuuzi na kusema uongo?
3 Jueni kuwa Mwenyezi-Mungu amejiteulia mwaminifu wake.Mwenyezi-Mungu husikia kila ninapomwomba.
4 Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi;tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.
5 Toeni tambiko zilizo sawa,na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.