4 mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,binadamu ni nini hata umjali?
5 Umemfanya awe karibu kama Mungu,umemvika fahari na heshima.
6 Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote;uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake:
7 Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini;
8 ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.
9 Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,kweli jina lako latukuka duniani kote!