5 Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha;mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi,na kulalia nguo za magunia na majivu.Je, huo ndio mnaouita mfungo?Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
6 “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:Kuwafungulia waliofungwa bila haki,kuziondoa kamba za utumwa,kuwaachia huru wanaokandamizwa,na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
7 Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
8 “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko,mkiwa wagonjwa mtapona haraka.Matendo yenu mema yatawatangulia,nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
9 Ndipo mtakapoomba,nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia;mtalia kwa sauti kuomba msaada,nami nitajibu, ‘Niko hapa!’“Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu,mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,
10 mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa,mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki,mwanga utawaangazia nyakati za giza,giza lenu litakuwa kama mchana.
11 Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima,nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida.Nitawaimarisha mwilini,nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji,kama chemchemi ya majiambayo maji yake hayakauki kamwe.