7 Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
8 “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko,mkiwa wagonjwa mtapona haraka.Matendo yenu mema yatawatangulia,nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
9 Ndipo mtakapoomba,nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia;mtalia kwa sauti kuomba msaada,nami nitajibu, ‘Niko hapa!’“Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu,mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,
10 mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa,mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki,mwanga utawaangazia nyakati za giza,giza lenu litakuwa kama mchana.
11 Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima,nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida.Nitawaimarisha mwilini,nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji,kama chemchemi ya majiambayo maji yake hayakauki kamwe.
12 Magofu yenu ya kale yatajengwa;mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani.Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta,watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.
13 “Kama ukiacha kufanya kazi siku ya Sabato,ukaacha shughuli zako siku yangu hiyo takatifu;kama ukiifanya siku yangu kuwa ya furaha,ukaiheshimu siku hiyo takatifu ya Mwenyezi-Mungu,ukaacha na shughuli zako na kupiga domo,