7 Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu.Mungu aliniambia:‘Wewe ni mwanangu,mimi leo nimekuwa baba yako.
8 Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako,na dunia nzima kuwa mali yako.
9 Utawaponda kwa fimbo ya chuma;utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’”
10 Sasa enyi wafalme, tumieni busara;sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia.
11 Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji;
12 msujudieni na kutetemeka;asije akakasirika, mkaangamia ghafla;kwani hasira yake huwaka haraka.Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!