1 Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu,ni wengi mno hao wanaonishambulia.
2 Wengi wanasema juu yangu,“Hatapata msaada kwa Mungu.”
3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande;kwako napata fahari na ushindi wangu.
4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu,nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.