1 Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu,nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu.Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”
2 Nilikuwa kama bubu, bila kusema kitu,nilinyamaza lakini sikupata nafuu.Mateso yangu yalizidi kuwa makali,
3 mahangaiko yangu yakaniunguza moyoni.Kadiri nilivyowaza ndivyo nilivyotaabika,kisha maneno haya yakanitoka:
4 “Ee Mwenyezi-Mungu, unijulishe mwisho wangu,siku zangu za kuishi zimenibakia ngapi,nijue yapitavyo kasi maisha yangu!”
5 Kumbe umenipimia maisha mafupi sana!Maisha yangu si kitu mbele yako.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
6 Kweli, kila mtu anapita kama kivuli;jitihada zake zote ni bure tu;anakusanya mali, asijue atakayeipata!