7 Na sasa, ee Bwana, ninatazamia nini?Tumaini langu ni kwako wewe!
8 Uniokoe katika makosa yangu yote;usikubali wapumbavu wanidhihaki.
9 Niko kama bubu, sisemi kitu,kwani wewe ndiwe uliyetenda hayo.
10 Usiniadhibu tena;namalizika kwa mapigo yako.
11 Unapomwadhibu mtu dhambi zake kwa kumkemea,unaharibu kama nondo kile akipendacho.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
12 Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu;usikilize kilio changu,usikae kimya ninapolia.Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye,ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.
13 Uache kunitazama nipate kufurahi kidogo,kabla sijaaga dunia, na kutoweka kabisa.