1 Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,kweli jina lako latukuka duniani kote!Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu!
2 Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao,umejiwekea ngome dhidi ya adui zako,uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
3 Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako,mwezi na nyota ulizozisimika huko,
4 mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,binadamu ni nini hata umjali?