3 “Nyinyi mnaniuliza:‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni?Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’“Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga,mnatafuta tu furaha yenu wenyewe,na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!
4 Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi.Mkifunga namna hiyomaombi yenu hayatafika kwangu juu.
5 Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha;mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi,na kulalia nguo za magunia na majivu.Je, huo ndio mnaouita mfungo?Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
6 “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:Kuwafungulia waliofungwa bila haki,kuziondoa kamba za utumwa,kuwaachia huru wanaokandamizwa,na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
7 Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
8 “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko,mkiwa wagonjwa mtapona haraka.Matendo yenu mema yatawatangulia,nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
9 Ndipo mtakapoomba,nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia;mtalia kwa sauti kuomba msaada,nami nitajibu, ‘Niko hapa!’“Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu,mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,