1 Heri mtu yule asiyekwendaKatika shauri la wasio haki;Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwaKandokando ya vijito vya maji,Uzaao matunda yake kwa majira yake,Wala jani lake halinyauki;Na kila alitendalo litafanikiwa.
4 Sivyo walivyo wasio haki;Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.