1 Bwana ndiye aliye mkuu,Na mwenye kusifiwa sana.Katika mji wa Mungu wetu,Katika mlima wake mtakatifu.
2 Kuinuka kwake ni mzuri sana,Ni furaha ya dunia yote.Mlima Sayuni pande za kaskazini,Mji wa Mfalme mkuu.
3 Mungu katika majumba yakeAmejijulisha kuwa ngome.
4 Maana, tazama, wafalme walikusanyika;Walipita wote pamoja.
5 Waliona, mara wakashangaa;Wakafadhaika na kukimbia.
6 Papo hapo tetemeko liliwashika,Utungu kama wa mwanamke azaaye.
7 Kwa upepo wa masharikiWavunja jahazi za Tarshishi.
8 Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,Katika mji wa BWANA wa majeshi.Mji wa Mungu wetu;Mungu ataufanya imara hata milele.
9 Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,Katikati ya hekalu lako.
10 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia.Mkono wako wa kuume umejaa haki;
11 Na ufurahi mlima Sayuni.Binti za Yuda na washangilieKwa sababu ya hukumu zako.
12 Tembeeni katika Sayuni,Uzungukeni mji,Ihesabuni minara yake,
13 Tieni moyoni boma zake,Yafikirini majumba yake,Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.